Katika hotuba yake ya usiku kwenye mkesha wa Krismasi, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema kuwa Krismasi hii ya pili mfululizo wakati wa vita vya kujihami vya Ukraine dhidi ya Russia, kipengele muhimu zaidi kwa familia za wa-Ukrane, sio kwa ajili ya mlo gani uliopo mezani, lakini watu ambao wako mezani. Na kuna thamani gani kuwa nao karibu.
Zelenskyy alisema kuwa maadili na matarajio ya Wa-Ukraine yamebadilika tangu mwanzo wa vita. Inavyoonekana leo sio sana kuhusu jinsi tunavyopamba nyumba zetu, lakini zaidi tunavyowalinda na kuondoa fujo, kumuondoa adui nje ya nyumba yetu. Jinsi tunavyofurahi kuona nyota ya kwanza angani jioni na sio kuona makombora ya adui na mauaji ndani yake, alisema.
Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1917, Ukraine inasherehekea Krismas Desemba 25 badala ya Januari 7, tarehe ambayo Russia inasherehekea.