Uingereza inatoa wito wa mageuzi ya mahakama ya ulaya ya haki za binadamu

Mfano wa nembo inayohusu sheria

June mwaka jana majaji kwenye mahakama hiyo waliweka amri katika dakika za mwisho wakizuia ndege ya kwanza kuondoka. Mahakama ya ulaya ya haki za binadamu ni chombo cha mahakama ya baraza la ulaya, taasisi ya haki za binadamu yenye nchi wanachama 46 na sio sehemu ya umoja wa ulaya

Uingereza inatoa wito wa mageuzi ya mahakama ya ulaya ya haki za binadamu wakati serikali inajaribu kushinikiza kupitishwa sheria mpya ambao itawaruhusu wanaoomba hifadhi wanaowasili kwa boti ndogo ndogo kupelekwa haraka Rwanda kwa usaili na makazi,bila kuwa na haki ya kukata rufaa.

June mwaka jana majaji kwenye mahakama hiyo waliweka amri katika dakika za mwisho wakizuia ndege ya kwanza kuondoka. Mahakama ya ulaya ya haki za binadamu ni chombo cha mahakama ya baraza la ulaya, taasisi ya haki za binadamu yenye nchi wanachama 46 na sio sehemu ya umoja wa ulaya.

Kumekuwa na ongezeko la haraka la idadi ya wahamiaji wanaowasili kwa boti ndogo kwenye ufukwe wa Uingereza kutoka Ufaransa katika miaka ya hivi karibuni. Serikali ina matumaini kwamba azma ya kuwapeleka Rwanda, bila ya haki ya kurudi Uingereza, itawadhoofisha wahamiaji wengi wanaofanya safari hatari kukatisha mkondo wa Uingereza-English Channel.

Pia inaamini sera hiyo itapelekea kuvunja magenge ya wafanyabiashara ya usafirishaji haramu wa binadamu.