Uingereza inasema uhusiano wa kidiplomasia wa Russia na Iran umeimarika

Rais wa Russia Vladmir Putin (L) akiwa na mwenzake wa Iran Ebrahim Raisi

Msaada wa kijeshi wa Iran kwa Russia umejumuisha mamia ya mashambulizi ya upande mmoja ya  magari  ya angani ambayo yamekuwa sehemu muhimu ya kampeni ya Russia nchini Ukraine na hivi sasa yanatengenezwa kwa leseni maalum huko nchini Russia.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema Jumatatu katika ripoti yake ya kila siku ya ujasusi kuhusu uvamizi wa Russia kwa Ukraine kwamba uvamizi huo umesababisha kutengwa kimataifa, na kuilazimisha Russia “kuelekeza tena juhudi zake kwa sera za mambo ya nje” na kuunda ushirikiano na ushirika mdogo unaovutia kwa msaada wa kidiplomasia, kiuchumi na kijeshi.

Katika ripoti kwenye mtandao wa X, ambao zamani ulijulikana kama Twitter, wizara hiyo ilisema uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi wa Russia na Iran umeimarika tangu uvamizi huo ulipoanza.

Msaada wa kijeshi wa Iran kwa Russia umejumuisha mamia ya mashambulizi ya upande mmoja ya magari ya angani ambayo yamekuwa sehemu muhimu ya kampeni ya Russia nchini Ukraine na hivi sasa yanatengenezwa kwa leseni maalum huko nchini Russia.

Onyo jipya siku ya Jumapili kwamba Kremlin ipo tayari na itaendelea kutumia mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israeli ili kupenyeza maneno yake dhidi ya uingiliaji kati wa Magharibi nchini Ukraine, kuwavunja moyo Wa-Ukraine na kuwahakikishia Wa-Russia kwamba lengo la Magharibi juu ya mgogoro wa Israeli litaondoa umakini wake kutoka kwa vita nchini Ukraine, kulingana na Taasisi ya Utafiti wa Vita (ISW).

Kufuatia mashambulizi ya Hamas huko Israel hapo Oktoba 7, Kremlin kimsingi ililaumu Magharibi kwa kupuuza migogoro katika Mashariki ya Kati na kuunga mkono Ukraine na kudai kuwa jumuiya ya kimataifa itaelekeza umakini wake kwa mgogoro wa Mashariki ya Kati na itaacha kuzingatia suala la Ukraine.