Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumamosi katika taarifa yake ya kila siku ya ujasusi juu ya uvamizi wa Russia kwa Ukraine kwamba katika wiki iliyopita kumekuwa na mapigano makali ya ardhini katika maeneo matatu, mhimili wa Kupiansk huko Luhansk, Avdiivka huko Donetsk na kwenye ukingo wa kushoto wa Mto Dnipro huko Kherson, ambako vikosi vya Ukraine vimeweka daraja.
Wakati Russia ilipata vifo vingi kuzunguka Avdiivka, ripoti hiyo ilisema hakuna upande uliopata mafanikio makubwa katika maeneo yoyote. Hakuna uwezekano wa kuwa na mabadiliko yoyote makubwa katika maeneo hayo, wizara ya Uingereza ilionya wakati msimu wa baridi Ulaya Mashariki unaingia.
Rais wa Ukraine Volodomyr Zelenskyy amesema Ijumaa katika hotuba yake ya kila siku kwamba Ukraine itatafuta rasilimali kwa ajili ya ujenzi mpya wa vyuo vikuu vilivyoharibiwa na mashambulizi ya Russia.
Alisema alitembelea moja ya shule siku ya Ijumaa, ni Chuo Kikuu cha Jimbo la chuo Kikuu cha Serikali cha Mariupol, ambacho kimehamia Kyiv. Zelenskyy alisema chuo kikuu kinafanya kazi na kuweka imani katika Ukraine, kwa watu wetu, na katika imani kwamba Ukraine itakuwa huru. Gazeti la Moscow Times ambalo ni maarufu miongoni mwa wahamiaji wa Russia, liliongezwa Ijumaa katika orodha ya “mawakala wa kigeni” na wizara ya sheria ya Russia.
Hii ni nyongeza ya hivi karibuni katika ukandamizaji wa Russia unaoendelea dhidi ya vyombo vya habari na upinzani unaokosoa vita vyake nchini Ukraine.