Uhusiano kati ya India na Taiwan waonyesha dalili za kuimarika

Picha za bendera za Taiwan na India

Kwa kile ambacho kinaonekana kama dalili  ya kuimarika kwa mahusiano kati ya India na Taiwan, Taipei wiki hii imetangaza nia yake ya kuongeza uwepo wake nchini humo, kwa kufungua ofisi ya mwakilishi mjini Mumbai

Ingawa India imekuwa na uhusiano mdogo wa kisiasa na Taiwan, biashara kati ya mataifa yote mawili imekuwa ikiongezeka katika miaka ya karibuni. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya India Arindam Bagchi Alhamisi alisema kwamba mpango wa Taiwan wa kufungua kituo cha Mumbai unahitaji kutazamwa kwa muonekano wa sera ya India ya kuimarisha ushirikiano na Taiwan kwenye nyanja za biashara, utalii, utamaduni, elimu pamoja na utangamano wa moja kwa moja miongoni mwa watu na bidhaa. Wachambuzi wanasema kwamba hatua ya Taiwan inakuja wakati mataifa yote mawili yakishuhudia kushuka kwa ushirikiano wao na China.