Uganda yapitisha sheria kali dhidi jamii ya LQBTQ

Waandamanaji wa kutetea haki za mashoga Uganda. Picha ya maktaba.

Bunge la Uganda limepitisha mswada unaopendekeza kifungo cha hadi maika 10 jela kwa wapenzi wa jinsia moja kufuatia shinikizo kubwa la kuchukuliwa kwa hatua dhidi yao, hatua inayoonekana kuhujumu jamii ya mashoga kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa shirika la habri la AP, mswada huo imepitishwa Jumanne jioni ndani ya ukumbi wa bunge uliojaa baada ya Spika kuuliza kila moja kuhusu msimamo wao, akisema kwamba ilikuwa muhimu kujua iwapo kuna baadhi waliokuwa wanapinga. Hata hivyo mswada huo uliidhinishwa na karibu wabunge wote 389 waliokuwepo.

Muda mfupi baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Spika Anita Among aliwapongeza, akisema kwamba walichofanya ni kwa manufaa ya watu wa Uganda. Mswada wa awali sawa na huo 2014, ulipingwa na mahakama kwa misingi ya kimikakati.

Mswada huo sasa utapelekwa kwa Rais Yoweri Museveni ambaye ana mamlaka ya kukataa au kuidhinisha, ingawa hapo awali alisema kwamba alikiwa anaunga mkono. Mswada huo uliwasilishwa bungeni mwezi uliopita na mbunge wa upinzani, akisema kwamba lengo lilikuwa kuadhibu wanaofadhili na kueneza vitendo vya wapenzi wa jinsia moja, maarifu kama LGBTQ.