Bunge la Uganda linatarajiwa kuvunjwa wakati wowote kuanzia sasa ili kutoa fursa ya kuandaliwa kwa uchaguzi mwingine. Bunge hilo hata hivyo limeingia katika historia kwa kuunda sheria ambazo zimezua utata kote duniani ikiwemo sheria kali dhidi ya mashoga, kupiga marufuku sketi fupi kwa wanawake na ile ya kutaka waganda na kila mgeni anayeingia nchini humo kupimwa virusi vya ukimwi kwa lazima.
Bunge la Uganda kuvunjwa.
Mara kadhaa, wabunge walirushiana maneno, nusra wapigane, huku baadhi wakifukuzwa kutoka vikao vya bunge. Bunge hilo la tisa limeidhinisha na kupitisha miswada themanini na nne. Moja wapo wa miswada ilioleta sintofahamu ni ule wa uchimabaji mafuta ambao ulivutia hata hisia za Umoja wa Mataifa. La ajabu ni kwamba mswada unaoharamisha mkusanyiko wa watu zaidi ya wanane uliwasilishwa na aliekuwa waziri mkuu Amama Mbabazi ambaye sasa anawania kiti cha urais akiwa kwenye upinzani ambapo mikusanyiko ya watu ni muhimu.