Uganda kuwasaka waasi wa ADF DRC

Mkuu wa polisi wa Uganda Jenerali Edward Kale Kayihura

Kulingana na mkuu wa polisi wa Uganda generali Kale Kayihura, Jamhuri ya Congo imeficha makundi ya waasi wanaotishia usalama wa Uganda na ni heri yasambaratishwe kabla ya kutekeleza maafa Uganda.

Uganda imetishia kuingia nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kwa lazima na kuwasaka waasi wa Allied democratic forces -ADF.

Kulingana na mkuu wa polisi wa Uganda generali Kale Kayihura, Jamhuri ya Congo imeficha makundi ya waasi wanaotishia usalama wa Uganda na ni heri yasambaratishwe kabla ya kutekeleza maafa Uganda.

Your browser doesn’t support HTML5

uganda kufichua waasi congo

Amesema Uganda iko tayari na imejipanga kuhakikisha waasi wanafichuliwa kabla hawajavamia nchi yao.

Amesema ni vyema serikali za nchi hizo mbili kutambua hatari hiyo na kuchukua hatua za aharaka.