Uganda imepanga kuwatoza faini watu wote wanaokataa kuchanjwa dhidi ya COVID 19

Waziri wa afya wa Uganda Ruth Aceng kushoto.

Uganda imepanga kuwatoza  faini watu wote wanaokataa kuchanjwa dhidi ya COVID 19 na wale watakaoshindwa kulipa faini hiyo wanaweza kupelekwa jela chini ya sheria mpya ya afya ya umma ambayo wabunge wanaichunguza , bunge limesema Jumanne.

Uganda imepanga kuwatoza faini watu wote wanaokataa kuchanjwa dhidi ya COVID 19 na wale watakaoshindwa kulipa faini hiyo wanaweza kupelekwa jela chini ya sheria mpya ya afya ya umma ambayo wabunge wanaichunguza , bunge limesema Jumanne.

Ingawa nchi hiyo ya Afrika Mashariki ilianza kutoa chanjo za COVID-19 karibu mwaka mmoja uliopita, ni takriban milioni 16 tu ambazo zimetolewa katika idadi ya watu milioni 45, huku maafisa wakilaumu kusita kwa kasi kuwa kumepelekea watu wachache kupata chanjo.

Taarifa ya bunge ilimnukuu waziri wa afya Ruth Aceng akiwaambia wabunge katika kamati hiyo kwamba masharti ya lazima ya kuchanjwa yatahakikisha kuwa watu wengi wamepata chanjo ili kuwezesha kuwa na kinga ya umma.

Taarifa hiyo haijasema ni lini sheria mpya itapelekwa mbele ya wabunge wote kwa ajili ya kupitishwa.

Uganda inapanga kutoza faini kwa watu wanaokataa kupewa chanjo dhidi ya COVID-19 na wale ambao watashindwa kulipa wanaweza kufungwa jela chini ya sheria mpya ya afya ya umma ambayo wabunge wanaichunguza, bunge ilisema Jumanne.

Kamati ya afya ya bunge imeanza kuchunguza Muswada wa marekebisho ya Sheria ya Afya ya Umma wa mwaka 2021 ambao unalenga kufanya chanjo ya corona kuwa ya lazima.

Sheria hiyo mpya inapendekeza kutozwa faini ya shilingi milioni 4 za Uganda kwa wale ambao watashindwa kupata chanjo.