Kupitia barua kutoka kwa wizara ya mambo ya nje kwa shirika la UN la haki za binadamu mapema mwezi huu, Uganda imesema kwamba hatua hiyo imepelekewa na maendeleo makubwa yaliopatikana katika uwezo wake wa kuhakikisha haki za binadamu nchini.
Mkuu wa shirika hilo la OHCHR, tawi la Uganda Bernard Amwine, amewaambia shirika la habari la Reuters kwamba hana tamko lolote kufuatia hatua tangazo hilo. Serikali ya rais Yoweri Museveni kwa miaka mingi imetuhumiwa na upinzani , mashirika ya kutetea haki za binadamu pamoja na baadhi ya mataifa ya magharibi kwa ukiukaji wa haki za binadamu, kushikilia watu kinyume cha sheria pamoja na mauaji kutoka kwa maafisa wa usalama.
Hata hivyo serikali imekuwa ikikanusha madai hayo na badala yake kusema kwamba wale wanatotuhumiwa wameadhibiwa kwa mujibu wa sheria. Museveni mwenye umri wa miaka 78 ametawala Uganda tangu 1986 wakati upinzani ukidai kwamba anamtayarisha mwanawe ambaye ni jenerali wa jeshi kuchukua usukani baada yake, madai ambayo ameendelea kukanusha.