Akiwasili kwa mazungumzo na mawaziri wengine wa fedha wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels, Le Maire alielezea uamuzi huo ulikuwa wa "kihistoria.” Vikwazo hivyo vipya vinamaanisha kuwa Russia itapoteza hadhi yake ya kuwa taifa linalothaminiwa zaidi kibiashara, na Umoja wa mataifa.
Le Maire amesema hii itaruhusu nchi za EU kuongeza ushuru kwa bidhaa zote za Russia.
"Hivyo ndivyo vikwazo vikali zaidi kuwahi kupitishwa na Umoja wa Ulaya, katika historia yake," alisema.
Hatua hizo mpya, ndizo za hivi punde kabisa, za Umoja wa Ulaya kuhusu vikwazo, tangu uvamizi huo uanze mwezi uliopita.
Tangu wakati huo, EU imeweka vikwazo dhidi ya Rais Vladimir Putin, mfumo wa kifedha wa Russia, na matajiri wenye ushawishi mkubwa nchini humo.
Umoja huo umeendelea kuweka vikwazo zaidi kwa watu 160, na kuongeza vikwazo vipya, kwa uchukuzi wa baharini na teknolojia ya mawasiliano ya redio.
.