Ufaransa na Mali zimesitisha utoaji wa viza kwa raia wa nchi hizo katika mzozo ambao tayari umesababisha kuondoka kwa jeshi la Ufaransa kutoka kwa mshirika wake wa zamani wa Sahel, wanadiplomasia wamesema Alhamisi.
Ubalozi wa Ufaransa mapema wiki hii ulisitisha kwa muda utoaji wa viza mpya katika mji mkuu wa Mali, Bamako baada ya kuiweka nchi hiyo katika eneo hatarishi ambapo imeshauri raia wake kutokwenda huko.
Serikali ya kijeshi ya Mali ilijibu kwa kuzuia visa mpya kwa raia wa Ufaransa katika ubalozi wake mjini Paris kitendo cha kujibu kile kilichoanywa na Ufaransa, wizara ya mambo ya nje ya Mali imesema. Agosti 7, wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ilitoa taarifa mpya juu ya mwongozo wake wa kusafiri.
Katika muktadha wa hivi sasa wa mivutano mikali ya kikanda safari zote za kwenda Mali zimezuiliwa. Raia wa Ufaransa nchini Mali wanaombwa kuwa makini zaidi, ilisema taarifa hiyo.