Mwaka 2023 hadi sasa haujawa mzuri kwa Afrika. Mgogoro uliozuka nchini Sudan, umezidi kuongezeka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuenea kusini kutoka Sahel.
Hali mbaya ya hewa, mara nyingi ihusishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, ambayo yamesababisha ukame mbaya pamoja na mafuriko katika maeneo kama Kenya na Sudan Kusini na kuongeza umaskini.
Uchumi wa nchi nyingi za Afrika unakabiliwa na madeni makubwa. Lakini mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anapendelea kuzingatia ahadi ya bara hilo; hasa, jinsi ya kutumia vizuri mali zake kutokana na utajiri wake mkubwa wa maliasili hadi nguvu kazi yake kubwa, na ya vijana kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, kuwekeza katika maendeleo endelevu na uchumi wa kijani kukua.
“Nimekuwa nikishinikiza kwamba tunahitaji kuzithamini nchi zetu kulingana na mtaji wao wa asili,” Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Akinwumi Adesina, aliiambia VOA wakati wa ziara yake ya hivi karibuni mjini Paris.