Hatua hiyo ni kutokana na madai kwamba walihusika katika udanganyifu pamoja na masuala mengine ya kuvuraga zoezi hilo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, miongoni mwa walioathiriwa ni pamoja na wagombea wa mabaraza ya majimbo na manispaa, na ambao matokeo yao bado hayajatangazwa.
Hata hivyo taarifa hiyo ya Ijumaa kutoka tume ya uchaguzi ya CENI, haikutaja lolote kuhusiana na uchaguzi wa rais uliozua utata pia, baada ya Rais Felix Tshisekedi kutangazwa mshindi Jumapili iliyopita. Upinzani umepinga matokeo hayo ukidai kwamba kulikuwa na dosari nyingi wakati wa zoezi hilo.
Hatua hiyo inahofiwa kuyumbisha zaidi taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa madini, na ambalo tayari limetatizika.