Rais wa Marekani, Donald Trump amesema wiki ijayo atamteua mwanamke kuchukua nafasi ya jaji wa mahakama ya juu merehemu Ruth Bader Ginsburg, na hivyo kuzusha malumbano ya kisiasa juu ya mrithi wake.
Ginsburg ambaye alikuwa na umri wa miaka 87, alifariki Ijumaa wiki kadhaa kabla ya uchaguzi war urais.
Hasimu wa kisiasa wa Trump, Mdemoract Joe Biden, amesisitiza uamuzi wa kujaza nafasi hiyo usubiri mpaka baada ya uchaguzi.
Kiitikadi uwiano wa majaji katika mahakama hiyo ya juu ni muhimu sana kwa maamuzi yake muhimu katika sheria za Marekani.
Nitawasilisha jina mteuzi wangu wiki ijayo Trump amesema katika mkutano wake wa kampeni huko Fayettevile North Carolina siku ya Jumamosi.
Kwa hakika nitamteua mwanamke kujaza nafasi hiyo kwa sababu nawapenda wanawake zaidi kuliko wanaume ameongezea.