Donald Trump Alhamisi amemfungulia mashtaka mpinzani wake katika uchaguzi wa urais wa Marekani wa 2016, Hillary Clinton, na Wademokrat wengine kadhaa, akidai kuwa walijaribu kufanya wizi wa uchaguzi kwa kuihusisha kampeni yake na Russia.
Mashtaka hayo yanahusiana na orodha ndefu ya malalamiko ambayo rais wa zamani Mrepublikan amerejea kuyatangaza wakati wa utawala wake wa miaka minne White House baada ya kumshinda Clinton, na yanakuja wakati akiendelea kutoa madai ya uongo kuwa uchaguzi wake wa 2020 alioshindwa na Rais Mdemokrat Joe Biden ulikuwa umetokana na wizi wa kura.
“Hadharani, washtakiwa walifanya hujuma yenye hila kutengeneza maelezo ya uongo kuwa mpinzani wao Mrepublikan, Donald J. Trump, alikuwa anashirikiana na taifa adui la kigeni,” rais wa zamani alidai katika mashtaka ya kurasa 108 aliyofunguwa katika Mahakama ya serikali kuu huko Florida.
Kesi hiyo ina madai “uhalifu uliopangwa” na “hujuma yakusababisha uongo wenye madhara,” kati ya
Mwakilishi wa Clinton hakujibu alipotakiwa atoe maoni yake kuhusu hayo.
Kesi hiyo inataka fidia na adhabu ya uharibifu. Trump alisema “alilazimishwa kutoa gharama kwa kiwango kitakacho amuliwa na mahakama, lakini inajulikana kuwa ni kiwango kinachozidi dola ($24,000,000) na inaendelea kujilimbikiza, katika namna ya gharama za ulinzi, gharama za kisheria, na gharama nyingine.