Timu ya Uganda City Oilers ilijikuta inaanguka kwa mara ya pili baada ya kufungwa na mabingwa wa Guinea SLAC kwa jumla ya pointi 96 kwa 68.
Mchezaji Uchenna Iroegbu wa SLAC alifunga pointi 22, wakati Ibrahima Fofana alipachika pointi 14, reboundi 6 na asisti 5, na S.L.A.C ya Guinea ikaizamisha City Oilers ya Uganda Jumanne usiku.
Ulikuwa ushindi wa kwanza kwa S.L.A.C katika michezo mitatu na watajaribu kubadilisha bahati yao katika michezo yao miwili ijayo. Mpinzani wao ajaye atakuwa Petro de Luanda wa Angola Jumatano jioni.
Wakati huo huo, City Oilers wakiongozwa na James Justice Jr. ambaye alimaliza na pointi 30 na kwa mara nyingine alikuwa mfungaji bora wa timu hiyo. Naye mchezaji Falando Jones aliongeza pointi 20 kwa Oilers ambao hawajashinda mchezo wowote mpaka sasa. Watacheza na CFV-Beira ya Msumbiji katika mechi yao ijayo.
Al Ahly ya Misri waingusha Cape Town Tigers ya Afrika kusini
Katika mchezo mwingine timu ya Al ahly ya Misri ilitoka na ushindi dhidi ya Caetown Tigers ya Afrika Kusini kwa jumla ya pointi 91 kwa 75.
Mchezaji Anunwa Omot wa Al Ahly alipachika pointi 28 na rebaundi 6, huku wachezaji wengine wanne wakichangia kwenye ubao wa matokeo, na Al Ahly ya Misri ikaibuka na ushindi dhidi ya Cape Town Tigers ya Afrika Kusini Jumanne usiku. Al Ahly bado haijashindwa katika kanda ya Nile na itamenyana na viongozi wa kanda hiyo Petro de Luanda Ijumaa usiku.
Evans Ganapamo aliiongoza Tigers kwa pointi 26, na Michael Gbinije na Samkelo Cele kwa pamoja walipachika pointi 30 na reboundi 10. Kwa ushindi mmoja katika michezo mitatu, Cape Town kwa sasa ni ya nne katika kanda ya Nile na itamenyana na CFV-Beira Jumatano jioni.