Tetemeko la ardhi laua 14 Papua New Guinea

Papua New Guinea

Watu 14 walifariki Jumanne katika maporomo ya ardhi na kuvunjika kwa majengo wakati wa tetemeko kubwa la ardhi katika eneo la ndani nchini papua new guinea, polisi na mfanyakazi wa hospitali walisema jumanne huku ripoti ambazo hazikuthibitishwa zikitaja idadi ya waliokufa kuwa 30.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, tetemeko hilo la kiwango cha 7.5 kwa kipimo cha rikta lilipiga katika eneo hilo mapema jana na kuharibu miundo mbinu ya madini na nishati na kupelekea kampuni ya Exxonmobil kufunga kiwanda chake cha gesi ya asili LNG. Nchi hiyo ni muuzaji mkubwa wa gesi.

"Majengo mawili yalianguka na maporomoko ya ardhi yalisababisha vifo vya watu katika eneo la mendi mji mkuu wa jimbo la Southern Highland," alisema muuguzi katika hospitali ya serikali ya mendi ambako miili ilipelekwa ili kuhifadhiwa.