Tanzania: Sumaye asema upinzani utaleta mabadiliko

Mkutano wa UKAWA Jangwani kuzindua kampeni yake

Vyama vyote vya kisiasa viko katika harakati za kujinadi kusaka kura kwa wananchi nchi nchima Tanzania vikitumia mbinu mbalimbali.

Joto la kisiasa nchini Tanzania linazidi kupanda huku wanasiasa wakijitokeza waziwazi kujinadi kwa ajili ya kusaka kura katika uchaguzi mkuu ujao Octoba 25.

Shutuma za rushwa zimezungumziwa sana na baadhi ya wagombea wanaojinadi kwa wananchi ili wawapigie kura.

Lakini viongozi mbalimbali wametoka katika vyama vyao vya kisiasa kama vile chama cha mapinduzi CCM na kuhamia kwenye muungano wa vyama vya siasa vya upinzani –UKAWA , na wengine pia wamehama upinzani kwenda CCM. sauti ya Amerika -VOA imefanya mahojiano na aliyekuwa waziri mkuu wa zamani Fredrick Sumaye nae anaeleza.

Your browser doesn’t support HTML5

Sumaye: Nimeenda Upinzani kwa Kutaka Mabadiliko

Uchaguzi mkuu wa mwaka huu umeonekana kuchukua sura na mwelekeo tofauti huku mwamko wa kisiasa ukishika kasi kwa wazee na hata vijana.