Vyama vyaonywa kuepuka matamshi hatari

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Tanzania Damian Lubuva

Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Tanzania Vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi huo vimeonywa kuepuka kampeni zitakazo hatarisha amani na mshikamano wa nchi.

Your browser doesn’t support HTML5

Vyama vyatakiwa kudumisha amani

Kampeni zinazokatazwa wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu ni za kutumia lugha za uchochezi, kejeli na matusi ambazo zinachochea kuvunjika kwa amani wakati wa upigaji kura au baada ya matokeao kutangazwa.

Jaji Francis Mutungi - msajili vya vyama vya siasa Tanzania, amesema amelazimika kutoa tahadhari hiyo kutokana na kushuhudia lugha na matendo yasiyofaa kutoka kwa baadhi ya vyama vinavyoshiriki uchaguzi mkuu ujao

Edward Lowassa mgombea urais wa Ukawa katika mkutano wa hadhara


Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam hii Jumatatu msajili huyo wa vyama vya siasa nchini hata hivyo alianisha kwamba jukumu kubwa la kufuatilia mwenendo wa kampeni za uchaguzi nchini ni la tume ya taifa ya uchaguzi

Vyama vinane vya saisa vinashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu nchini Tanzania lakini ushindani mkubwa katika kampeni upo kwa vyama viwili vya CCM na CHADEMA chini ya mwavuli wa umoja wa katiba ya waanchi UKAWA