Tanzania imetangaza kifo cha raia wake aliyeuawa kufuatia mapigano huko Israel

Tanzania imetangaza kifo cha raia mmoja aliyeuawa huko Israel kufuatia mapigano yanayoendelea kati ya Israel na Hamas

Serikali ya Israel imewataja wanafunzi wawili kutoka Tanzania, ambao ni Clemence Felix Mtenga mwenye miaka 22, na Joshua Loitu Mollel mwenye miaka 21, miongoni mwa watu 240 waliochukuliwa kwenda Ukanda wa Gaza

Tanzania imetangaza kifo cha raia mmoja kati ya wawili waliokuwa wakishikiliwa mateka na Hamas wakati wa mashambulizi ya Oktoba 7 huko Israel.

Serikali ya Israel imewataja wanafunzi wawili kutoka Tanzania, ambao ni Clemence Felix Mtenga mwenye miaka 22, na Joshua Loitu Mollel mwenye miaka 21, miongoni mwa watu 240 waliochukuliwa kwenda Ukanda wa Gaza.

“Ni kwa masikitiko makubwa tunathibitisha kifo cha Clemence Felix Mtenga”, taarifa ya wizara ya mambo ya nje ilisema Ijumaa jioni. Haikusema jinsi Mtenga alivyokufa. “Tunapenda pia kuufahamisha umma kwamba Joshua bado hajulikani alipo huku pia tunaendelea kufuatilia suala hilo”, wizara hiyo ilisema.

Israel imeapa kuliangamiza kundi la Hamas kufuatia mashambulizi ya Oktoba 7 ambayo maafisa wa Israel wanasema yaliua takriban watu 1,200 wengi wao wakiwa raia na walishuhudia kutekwa takriban watu 240.