Takriban watu 30 wapigwa risasi wakati wa sherehe mjini Baltimore

Taka zilizobaki kwenye eneo la sherehe amabako watu walipigwa risasi mjini Baltimore, Maryland, Jumamosi.

Maafisa wa Baltimore, Maryland wamesema kwamba takriban watu wawili wameuwawa na wengine 28 kujeruhiwa baada ya kupigwa risasi wakati wa sherehe kwenye mtaa wa kusini mwa mji huo wa Brooklyn Homes.

Ripoti za polisi zimesema kwamba watatu miongoni mwa waliojeruhiwa wapo katika hali mahututi.

Meya wa Baltimore Brandon Scott ameambia shirika la habari la CNN kwamba tukio hilo linaangazia umuhimu wa kushughulikia tatizo la umiliki wa bunduki, na siyo mjini humo pekee mbali kote nchini.

Kaimu mkuu wa polisi wa Baltimore Richard Worley amesema kwamba eneo la tukio halikai vizuri, akiongeza kuwa watu 20 miongoni mwa waliojeruhiwa waliweza kutembea wenyewe hadi hospitalini.

Meya Scott ametoa hotuba akisema kwamba hawatapumzika hadi wapate waliotekeleza ukatili huo. Ameongeza kwamba anatumia wanafikiria kuhusu kila uhai waliotoa pamoja na maisha athari walioleta kwenye maisha ya watu.