Takriban watu 18 wauwawa kwenye mlipuko mjini Dhaka, Bangladesh

Watu wakusanyika karibu na eneo la mlipuko mjini Dhaka, Bangladesh, March 7, 2023.

Maafisa wa Bangladesh wamesema kwamba mlipuko mkubwa ndani ya jengo katika kitongoji chenye shughuli nyingi kwenye mji mkuu  wa Dhaka umeua takriban watu 18 Jumanne, na kujeruhi darzeni wengine, siku chache baada ya milipuko miwili  sawa na huo kutokea nchini humo.

Jumla ya vifo kutokana na milipuko yote mitatu kufikia sasa ni 28. Polisi wanasema kwamba mlipuko wa Jumanne umetokea kwenye kitongoji cha Siddik Bazar saa za jioni wakati wa msongamano mkubwa.

Takriban watu 140 wamelazwa kwenye hospitali ya dharura ya Medical College mjini Dhaka, kulingana na inspekta wa polisi wa kituo cha polisi cha hospitali hiyo, Bacchu Mia,wakati akizungumza na VOA, kuhusu watu waliolazwa kwenye hospitali hiyo .

Mkuu wa idara ya zimamoto mjini Dhaka, Dinmoni Sharma amesema kwamba shughuli za uokozi silisitishwa kutokana na usiku kuingia,zikipangwa kuendelea hivi leo.