Sudan, Sudan Kusini watia saini makubaliano

Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa, Ban Ki Moon

Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa, Ban Ki Moon amepongeza makubaliano ya mafuta kati ya Sudan na Sudan Kusini akisema ni hatua muhimu sana katika kujenga uhusiano mzuri baina ya nchi hizo mbili

Baada ya miezi kadhaa ya mashauriano, nchi hizo zimekubaliano sudan kusini iilipe sudan chini ya dola tisa na nusu kwa pipa ili kusafirisha mafuta kupitia mabomba ya kaskazini.

Sudand kusini imefunga uzalishaji mafuta tangu mwezi january kwasababu ya mzozo. Mpatanishi wa kusini, pagan amum amewaambia waandishi wa habari jana kwamba uzalishaji huenda ukaanza tena mwezi ujao.

Katika taarifa kupitia kwa msemaji wake jana jumatatu, bwana ban amesema ametiwa moyo na serikali hizo mbili ambazo zimepunguza tofauti zao katika masuala mazito, ingawaje anasema anasikitishwa kwamba sudan hizo mbili hazikutimiza tarehe ya mwisho ya august mbili iliyowekwa na umoja mataifa kusuluhisha mizozo yote.

Majirani hao bado hawajasuluhisha mlolongo wa masual aya usalama, mpaka na uraia.
Bwana ban pia ameipongeza sudan kwa kutia saini waraka wa maelewano ambao utaruhusu misaada kuwafikia raia katika majimbo ya blue nile na kordofan kusini, ambako majeshi ya sudan yamekuwa yakipambana na waasi.