Mashirika ya haki za binadamu yanaeleza wasiwasi wao juu ya hatua kali za Sudan dhidi ya waandamanaji wanaopinga serikali ya nchi hiyo katika maandamano yalioanza tangu Desemba mwaka jana. Mashirika hayo yanasema hatua hiyo imepelekea watu 60 kufariki dunia na mamia kufungwa jela.
Kuongezeka kwa bei ya mkate na mafuta ya petroli kulipelekea maandamano ya awali ambayo yaliongezeka haraka na kudai kuondoka madarakani kwa rais wa muda mrefu wa nchi hiyo Omar al-Bashir.
Mkurugenzi wa Human Rights Watch (HRW) kitengo cha Afrika Jehanne Henry, amesema ukandamizaji mkubwa unaofanywa na polisi wa Sudan unalenga wapinzani, wanaharakati na waandishi wa habari.