Kesi hiyo imegundulika kwa mgonjwa mwenye umri wa miaka 34 aliyerejea nchini humo hivi karibuni baada ya ziara kwenye taifa la Afrika ya Kati la Equatorial Guinea.
Mwanzoni alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya kibinafsi, lakini sasa amehamishiwa katika wodi maalum iliyotengwa kwenye hospitali ya La Fe Valencia kwa uchunguzi zaidi kulingana na maafisa wa afya.
Kulingana na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha CDC, ugonjwa wa Maburg husababishwa na virusi na kusababisha kuvuja damu miongoni mwa wanadamu na nyani na unaweza kusababisha vifo.
Maafisa wa Uhispania wamesema kwamba zaidi ya watu 200 nchini Equatorial Guinea wamegundulika kuwa na maradhi ya Marburg katika siku za karibuni.
Mapema mwezi huu, kesi mbili za maambukizi ya ugonjwa huo yalipatikana nchini Cameroon karibu na mpaka wake na Equatorial Guinea.
Shirika la Afya Duniani WHO linasema kwamba ugonjwa huo unaosbabishwa na virusi unaweza kusababisha vifo kwa asilimia 88 ya wagonjwa, ukiwa kwenye kundi moja na ule wa virusi vya Ebola.