Kila mbinu inafanywa ingawa mafisa wa kijeshi wamesema kwamba huenda ikawa vigumu kufika mahala walikopelekwa. Helikopta hiyo iliyokodishwa na UN ilikuwa ikipeleka dawa, wakati hitilafu za kimitambo zilipoilazimisha kutua kwa dharura karibu na kijiji cha Hindhere, kililochoko katikati mwa Somalia, na kinachodhibitiwa na wanamgambo.
Wanaume wawili raia wa Somalia pamoja na raia kadhaa wa kigeni ni miongoni mwa watu waliokuwa ndani ya helikopta hiyo, wengi wao walichukuliwa mateka na wanamgambo, maafisa wawili wa usalama wameiambia Reuters.
Haijabainika idadi kamili ya watu waliotekwa nyara, au iwapo baadhi yao walizeza kutoroka. Waziri wa Habari Daud Aweis ameiambia Reuters kwamba serikali imekuwa ikifanya juhudi za kuwaokoa tangu Jumatano, na kwamba juhudi hizo zinaendelea Ahamisi.