Ni mwaka mmoja sasa tangu serikali ya Sierra Leone kutangaza kuwa ugonjwa wa Ebola ni suala la dharurua la kitaifa .
Mwezi September, Marekani ilibuni mfumo wa muda mfupi kukidhi mahitaji ya kupambana na virusi hivyo hatari, ambavyo viliuwa Zaidi ya watu elfu 11 kote huko Africa Magharibi.
Mfumo huo ujulikanoa kama UNMEER ni mfumo wadharura wa umoja mataifa wa kupambana na virusi vya Ebola.
Ujumbe huo unamaliza shughuli zake huko Sierra Leone mwishoni mwa wiki hii ya mwezi Julai.
Ripoti mpya kutoka shirika la afya la umoja wa mataifa - WHO, inaeleza idadi ya kesi za kila wiki za Ebola kuwa chini huko Sierra Leone na Guinea.
Vita dhidi ya Ebola hata hivyo, bado havijaisha . Kuna wasiwasi juu ya kifo cha hivi karibuni kutokana na Ebola katika wilaya ya Tonkolili huko kaskazini mwa nchi.
Mwanamume mmoja ambaye amekuwa akiuza mayai huko Freetown na baadae kusafiri hadi Tonko aliuugua na baadae kufariki.
Virusi vya Ebola vilithibitishwa baada ya majaribio ya vipimo. Wilaya hiyo hapo awali ilifisha siku 150 bila kuwa na kesi ya ebola na maafisa wanasema kesi hii inaweza kusababisha athari ya maambukizo mengine.