Shambulio la bomu na bunduki lililolenga hoteli moja katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, Jumatatu liliwaua washambuliaji wasiopungua watatu na kuwajeruhi watu wengine 21, wakiwemo raia wawili wa kigeni. Hoteli ya ghorofa kadhaa katika eneo la kibiashara la Shar-e Naw katikati ya mji mkuu wa Afghanistan ni makazi ya raia kadhaa wa China.
Msemaji wa serikali ya Taliban Zabihullah Mujahid amesema watu watatu wenye silaha walilivamia jengo hilo mchana kabla ya kujihusisha haraka na kuuawa na vikosi vya usalama. Alisema hakuna raia wa kigeni aliyeuawa.
"Hata hivyo raia wawili wa kigeni katika hoteli hiyo walijeruhiwa wakati wakiruka kutoka dirishani ili kuokoa maisha yao" Mujahid aliongeza. Hakufafanua zaidi.
Shirika la kimataifa la misaada ya kibinadamu linalojulikana kama EMERGENCY limeripoti idadi kubwa ya majeruhi likisema shambulizi hilo lilitokea umbali wa kilomita moja kutoka hospitali yake katika eneo hilo. "Kufikia sasa tumepokea majeruhi 21 huku watu watatu tayari walikuwa wamekufa walipowasili," shirika hilo la hisani lenye makao yake nchini Italia liliandika kwenye Twitter bila kufafanua