Serikali ya Sudan yaifahamisha IGAD kusimamisha uanachama wake

Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan akiwa Port Sudan August 27, 2023. Picha na REUTERS/Ibrahim Mohammed Ishak

Serikali ya Sudan iliyogubikwa na vita   imeifahamisha IGAD kwamba inasimamisha uanachama wake katika taasisi  hiyo ya Afrika Mashariki wizara ya mambo ya nje  iliyo chini ya jeshi Abdel Fattah al-Burhan ilisema  Jumamosi

Khartoum tayari ilitangaza Jumanne kwamba inasimamisha uhusiano na IGAD kwa kumwalika mkuu wa wanamgambo Mohamed Hamdan Daglo ambaye anapambana na Burhan kwa miezi tisa, kwenye mkutano uliofanyika nchini Uganda ambao ulijadili mzozo wa Sudan.


Sudan inakabiliwa na moja ya majanga yanayotokea kwa kasi duniani shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu, OCHA, linasema, huku zaidi ya watu milioni 7 wakiwa wameyahama makazi yao na zaidi ya nusu ya watu nchini humo wanahitaji misaada ya kibinadamu.