Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 49 amekuwa katika mivutano na serikali kwa zaidi ya miaka miwili sasa, hali iliyopelekea maandamano ya ghasia mara kadhaa nchini humo. Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, Sonko aliwasilisha ombi lake la kuwania urais kwenye uchaguzi huo wa Februari kwa baraza la katiba, licha ya serikali kumnyima stakabadhi zinazohitajika ili kushiriki zoezi hilo.
Serikali imesema kwamba mkutano wa kumteua Sonko uliopangwa kufanyika leo Jumamosi umepigwa marufuku kutokana na tishio la “ kuvuruga Amani ya umma, kuingilia kati uhuru wa watu kutembea pamoja na bidhaa na hatari ya ya kujiingiza kwa watu wenye nia mbaya, kulingana na amri iliyoonekana na AFP. Amri hiyo ilitiwa saini na mkuu wa usalama wa Dakar Cherif Mouhamadou Blondin Ndiaye, ambaye alithibitisha uhalali wake.