Scotland yaamua "HAKUNA" kujitenga

Matokeo ya mwisho baada ya wa-Scotland kupiga kura ya kutaka kuwa taifa huru, huko Edinburgh, Scotland, Sept. 19, 2014.

Wananchi wa Scotland wamepiga kura na kuunga mkono muungano wa miaka 307 baina ya nchi hiyo na Uingereza katika kura ya maoni ya kihistoria iliyokuwa ikisubiriwa kuamua iwapo Scotland itajitenga.

Matokeo yanaonyesha kwamba asilimia 55 ya wapiga kura walipendelea kuendelea kuwa sehemu ya Uingereza ikilinganishwa na asilimia 45 ambao walipiga kura ya kutaka kuwa taifa huru linalojitawala lenyewe.

Huko Glascow, mji mkubwa kabisa wa Scotland asilimia 61 ya wapiga kura walichagua “Ndio” kuunga mkono umoja uliopo kuendelea kuwa hai na asilimia 39 walipiga kura kuupinga umoja huo. Hata hivyo wapiga kura katika mji mkuu wa Scotland, Edinburgh na Aberdeen mji wa tatu kwa ukubwa nchini humo ulikataa kuwa taifa linalojitawala lenyewe kwa wingi mkubwa wa kura.

“Watu wa Scotland wamezungumza. Tumechagua umoja dhidi ya mgawanyiko na mabadiliko chanya kuliko mgawanyiko usio na maana”.

Katika hotuba inayoelezea kushindwa kwake, kiongozi wa kitaifa wa Scotland, Alex Salmond aliita kura ya maoni tathmini ya utaratibu wa kidemokrasia na aliwasihi wafuasi wanaotaka Scotland kujitenga kukubali matokeo ya kura.

“Watu wengi wa Scotland wameamua kupiga kura ya hapana kwa kipindi hiki, kutokuwa taifa huru. Ninakubali matakwa hayo ya watu na ninatoa mwito kwa wa-Scotland wote kufuata sheria katika kukubali matakwa ya demokrasia ya watu wa Scotland”.