“ Tumebakisha makamanda wachache tu, kiasi cha kuwahesabu kwa vidole.” Anasikika akisema Shabab al Muhajir anayesemakana kuwa kiongozi wa Islamic State Khorasan, au ISIS-K, akitumia lugha ya Pashto kwa wafuasi wake.
Kiongozi huyo pia anazungumzia mauaji ya baadhi ya viongozi wake kwenye kampeni ya hivi karibuni ya Taliban dhidi ya operesheni za kigaidi za ISIS-K, kwenye maficho yao mjini Kabul na kwingineko nchini.
Chombo cha habari cha The al Mersaad kilichotoa taarifa hizo kimetajwa na maafisa wa Taliban kwamba kinahusika katika kunapinga propaganda za kigaidi za ISIS-K.
Kufikia sasa hakuna tamko lolote kutoka ISIS-K kufuatia taarifa hizo. VOA bado haijaweza kudhibitisha iwapo sauti inayosikika ni ya kiongozi anayedaiwa kuwa wa ISIS-K.