Saudi Arabia yashtua ulimwengu wa soka

FIFA World Cup Qatar 2022

Saudi Arabia imeshtua Ulimwengu wa soka katika kombe la Dunia 2022 nchini Qatar kwa kuichapa Argentina  mabao 2-1 siku ya Jumanne.

Saudi Arabia imeshtua Ulimwengu wa soka katika kombe la Dunia 2022 nchini Qatar kwa kuichapa Argentina mabao 2-1 siku ya Jumanne.

Juhudi za Messi kupata taji kubwa duniani kwa wasi wasi kwa kurudisha kukumbu za kushindwa kwa bao 1-0 dhidi ya Cameroon katika kikosi cha Argentina iliyoongozwa na Diego Maradona katika mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Dunia la 1990.

Mabao ya Saleh Alshehri na Salem Aldawsari katika muda wa dakika tano katika kipindi cha pili yaliwapa Wasaudi ushindi. Argentina walichukua uongozi wa mapema kwa penalti kunako dakika ya 10 iliyofungwa na Lionnel Messi.

Matokeo mengine ya kushtusha katyika kombe la dunia ni kama vile ushindi wa bao 1-0 wa Senegal dhidi ya mabingwa watetezi Ufaransa katika mechi ya ufunguzi wa mashindano ya mwaka 2002 na pia Marekani kuifunga Uingereza kwa idadi hiyo hiyo ya magoli mwaka1950.

Mbio za Argentina za kutoshindwa mechi 36 ziliishia kwenye Uwanja wa Lusail katika mechi ya tano ya Messi na huenda ikawa ya mwisho katika Kombe la Dunia.Mambo yamebadilika.

Mfalme salman atangaza siku kusheherekea

Kwingineko kwa mujibu wa Saudi Gazzette Mfalme Salman wa Saudia Arabia ameagiza kwamba Jumatano, itakuwa likizo kwa wafanyakazi wote katika sekta za umma na binafsi pamoja na wanafunzi wote katika kusherehekea ushindi mnono wa SaudiArabia dhidi ya Argentina kwenye kombe la Dunia. Hiyo ni shughuli kweli kweli huko itaendelea.

Mexico yatoka suluhu na Poland

Timu ya taifa ya Mexico imepata oointi moja baada ya kutoka suluhu na Poland katika Mexico .

Golikipa mkongwe wa Mexico Guillermo Ochoa mwenye umri wa miaka 37 aligeuka shujaa wa mchezo huo baada ya kuokoa penati kunako dakika ya 58. Na kuondoa pentai ya mkongwe Lewandowski anatisha kweli kweli.

Ufaransa yatamba

Wakati huo Vijana wa Leu Bleu Timu ya taifa ya Ufaransa wamepata ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Australia katika mchezo mkali na wa kusisimua.

Australia ambao walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza mapema katika mchezo huo lakini Uffaransa walisawazisha bao hilo na kuongeza mengine matatu.

Ufaransa walicheza kewa ustadi mkubwa wakitengeneza naafasi na kukosa mabnao kadhaa. Kwa upande mwingine ngome ya Australia ilizuia mashambulizi mengi bila ya hivyo magoli yangeweza kuwa mengi zaidi.

Na katika mchezo mwingine wa kundi D timu ya taifa ya Tunisia -Carthage Eagles ilijipatia pointi moja mbele ya vijana wa Denmark baada ya kutoka sare 0-0 katika uwanja wa Al Rayan huko Education City.

Tunisia ilipambana kwa kiasi kikubwa na vigogo wa Denmark waliofika katika nusu fainali ya kombe la Ulaya na mpira ulikuwa mkali na wa kusisimua.

Washabiki wa Tunisia katika eneo la Souq Wakif mjini Qatar walisikika wakishangilia sana matokeo ya timu yao.