Rwanda yasitisha safari zake za ndege Kusini mwa Afrika

Your browser doesn’t support HTML5

Rwanda imesimaisha kwa muda safari zake za ndege kati ya Rwanda na nchi za Kusini mwa Afrika kufuatia maambukizo ya aina mpya ya kirusi kipya cha COVID-19 Omicron.

Nchi hiyo pia imeweka masharti ya kujiweka karantini kwa siku saba kwa wasafiri wote wanaowasili Kigali ambao hivi karibuni walikuwa katika nchi zilizoathiriwa na corona.