Kwenye ripoti ya kiintelijensia ya kila siku kutoka wizara hiyo huhusiana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine, wizara hiyo imesema kwamba wafungwa kadhaa waliosamehewa wataendelea kuhudumu kama mawakala kwenye kundi la Wagner, na kwamba Russia sasa hivi inadhibiti mfumo wa kuwatumia wafungwa hao.
Kundi la Wagner mwezi uliopita lilifanya jaribio la mapinduzi dhidi ya utawala wa Rais Vladimir Putin. Kusitishwa kwa program ya kutumia wafungwa kutoka kundi hilo kutafikisha kikomo moja wapo ya vipindi hatari zaidi katika historia ya kijeshi nchini Russia.
Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema kwamba hadi mamluki 20,000 wameuwawa ndani ya miezi michache iliyopita. Mkuu wa idara ya CIA William Burns amesema Alhamisi kwenye kikao cha Usalama cha Aspen cha kitaifa hapa Marekani kwamba huenda Putin anavuta muda kabla ya kulipiza kisasi dhidi ya kiongozi wa Wagner Yevgeny Prigozhin kutokana na jaribio hilo la mapinduzi.