Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali katika Bunge la Jamumuhi ya Muungano wa Tanzania, imewasilisha ripoti ya uchunguzi wa kashfa ya IPTL na kuhusisha uchotwaji wa shilingi bilioni 306 za kitanzania.
Pamoja na kuwepo tetesi za pingamizi ya mahakama kuzuia kusomwa kwa ripoti hiyo Bungeni, Mwenyeti wa kamati Zitto Kabwe alisoma ripoti na kulithibitishia Bunge hilo kwamba viongozi na wafanyakazi wa Serikali, wafanyabiashara, viongozi na taasisi za dini, mabenki na watu binafsi wanahusika kufanya katika ufisadifu.
Your browser doesn’t support HTML5
Mwenyekiti Kabwe pia ameliambia Bunge kwamba, kwa kutumia njia zisizo halali, watu hao walifanikiwa kutoa fedha kutoka akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania, iliyofunguliwa baada ya mgogoro na kapuni ya ufuaji umeme ya IPTL na Tanesco.
Naye Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo ya Bunge Deo Filikunjombe, akisoma sehemu ya pili ya ripoti hiyo ya mapendekezo ya kamati, amesema wale wote waliohusika wawajibishwe.
Ameongoza kuwa kuwajibishwa huko ni pamoja na kufilisiwa kwa wahusika kwa mali zao kupigwa mnada na ikiwezekana hata zile za nje ya nchi.
Pia Filikunjombe, alitaka viongozi wote wa Serikali waliotajwa katika ufisadi huo wawajibike pamoja na watumishi wa Serikali kufukuzwa kazi. Bunge litaendelea kesho na inatazamiwa mjadala mkali kuzuka na baadhi ya viongozi wa Serikali waliotajwa kujiuzulu.