Ripoti mpya ya Johns Hopkins yasifu China kwa kuheshimu mpango wa kusaidia mataifa masikini kukabiliana na madeni

Naibu Rais wa Marekani Kamala Harris akihutubia vijana kwenye bustani ya Black Star , Accra, Ghana, on March 28, 2023.

Ripoti mpya iliyotolewa na watafitii kutoka chuo kikuu cha Johns Hopkins hapa Marekani imesema kwamba China imepata pointi zaidi katika kushughulikia kusaidia baadhi ya mataifa ya kiafrika yaliyolemewa na madeni.

Ripoti hiyo ni kutokana na tadhmini ya kina ya namna Beijing ilivyotekeleza program ya kusaidia kwenye madeni, maarufu Service Suspension Intitiative au DSSI inayolenga mataifa yalioelemewa kama vile Angola na Zambia.

Ukiangazia nchi tatu za Kiafrika, Kenya, Zambia na Angola, utafiti huo mpya unaonyesha jinsi jitihada za China za kukabiliana na madeni zilivyotofautiana, lakini unaonyesha kwamba, kwa ujumla, nchi zilitimiza wajibu wao.

Mpango wa DSSI ulianzishwa 2020 na IMF na Benki kuu ya Dunia wakati wa mwanzo wa janga la Corona, ukipendekeza kwamba mataifa 20 tajiri duniani- G-20 yasitishe kwa muda kukusanya madeni yao kutoka kwenye mataifa masikini duniani.

Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen na mkuu wa Benki ya dunia David Malpass hivi karibuni wamelaumu China kwa kuwa zingiti cha utekelezwaji wa program hiyo. Naibu waziri wa Marekani Kamala Harris wiki iliyopita alikuwa nchini Zambia wakati akiomba wakopeshaji wake, China ikiongoza, wajaribu kutadhmini upya mikopo yao .

Ubalozi wa China nchini Zambia hata hivyo umekashifu Yellen ukisema kwamba matamshi yake hana msingi wowote.