Kiongozi huyo alialikwa na mwenzake wa Misri ili kushiriki kwenye mazungumzo hayo, ambayo yatajikita zaidi kwenye kuenea kwa mzozo kati ya Israel na ukanda wa Gaza. Ofisi ya Rais ya Afrika Kusini imesema kwamba mkutano huo ni kuhusu misaada ya kibinadamu pamoja na kutoa wito wa kuanza tena kwa mazungumzo ya amani.
Taarifa zimeongeza kuwa Ramaphosa alikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu mashambulizi dhidi ya raia, watu kukoseshwa makazi pamoja na mzozo wa kibinadamu huko ukanda wa Gaza.
Awali Ramaphosa alisema yupo tayari kuwa mpatanishi kwenye mzozo huo, akiongeza kuwa taifa lake linaweza kuwa mfano wa uzoefu wa utatuzi wa mizozo barani Afrika na kwingineko.