Rais wa zamani wa Afrika kusini Frederik De Klerk afariki dunia

Your browser doesn’t support HTML5

Rais wa zamani De Klerki afariki akiwa na umri wa miaka 85

Rais wa zamani wa Afrika kusini mzungu Frederik De Klerk amefariki akiwa na umri wa miaka 85, taasisi yake imesema leo

Rais wa zamani wa Afrika kusini mzungu Frederik De Klerk amefariki akiwa na umri wa miaka 85, taasisi yake imesema leo.

De Klerk na rais wa kwanza mweusi wa Afrika kusini Nelson Mandela walipata wote Tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1993 kwa kuongoza mabadiliko makubwa kutoka kwa utawala wa wazungu walio wachache nchini humo.

Taasisi yake imesema alifariki baada ya kupambana na ugonjwa wa saratani.

De Klerk alitangaza alikutwa na maradhi ya saratani wakati wa kusherekea miaka 85 ya kuzaliwa kwake, ilikuwa tarehe 18 Machi mwaka huu.

Anakumbukwa zaidi kwa hotuba yake maarufu aliyoitoa tarehe 2 Februari mwaka 1990, akitangaza kuondolewa marufuku dhidi ya chama cha African National Congress (ANC) na vyama vingine vyavilivyokuwa vinatetea ukombozi.

Katika hotuba hiyo hiyo, aliamuru kuachiliwa kutoka jela kwa Mandela aliyekuwa akipinga ubaguzi wa rangi baada ya kifungo cha takriban miaka 27.