Mwishoni mwa Machi Rais wa zamani wa Taiwan, Ma Ying-jeou alifanya safari ya kihistoria nchini China na kuwa kiongozi wa kwanza wa zamani au anayehudumu wa Taiwan kutembelea China bara tangu mwaka 1949.
Ma ambaye alihudumu kutoka mwaka 2008 hadi 2016 alisema alitamani kutembelea ardhi za mababu zake katika mkoa wa Hunan na miji kadhaa ya China. Picha zilikuwa nyingi lakini umakini mkubwa ulielekezwa kwa matamshi yake juu ya uhusiano wa kipekee wa Taiwan na China na namna ambavyo nchi zote mbili ni sehemu ya “China moja”. Katika muda mchache uliopita matamshi yake yanaweza kuwa na mvuto kidogo.
Taiwani rasmi, ni Jamhuri ya China iliyopewa jina kwa serikali ambayo ilikimbia kwenye kisiwa hicho koloni la zamani la Japan katika kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya China mwishoni mwa miaka ya 1940.
Kwa familia nyingi za China ambazo ziliondoka kwenye serikali iliyoongozwa na chama cha KMT na kuziona pande hizo mbili kuwa nchi moja ilikuwa ndoto ya maisha iliyozuiliwa na siasa za vita baridi.