Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy anatarajiwa kuhutubia mkutano wa kila mwaka unaohusu usalama huko Munich leo Ijumaa kwa njia ya video.
Mwaka jana, waliohudhuria mkutano huo walimsihi Rais wa Russia Vladimir Putin kutoivamia Ukraine.
Mwaka huu mkutano huo unafunguliwa siku chache kabla ya maadhimisho ya Februari 24 ya uvamizi huo.
Zelenskyy alisema katika hotuba yake ya usiku kwamba watu 101 wameachiliwa kutoka mikononi mwa Russia siku ya Alhamisi.
"Kuidhibiti hali katika mstari wa mbele na kujiandaa kwa hatua zozote zitakazoongezeka za adui ni kipaumbele kwa siku zijazo," alisema. "Kusonga mbele na ukombozi zaidi wa ardhi yetu ni kipaumbele ambacho tunakiandaa kwa uangalifu," aliongeza.
Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema katika taarifa zake za kila siku za kijasusi kuhusu Ukraine kwamba Wizara ya Ulinzi ya Russia na mkandarasi wake binafsi "huenda wameathirika" majeruhi 175,000 hadi 200,000 tangu kuanza kwa uvamizi huo ambapo takriban watu 40,000 hadi 60,000 waliuawa ikiwakilisha "uwiano mkubwa wa wafanyakazi waliouawa".