Rais wa Uganda apinga hatua ya Benki ya Dunia kusitisha ufadhili mpya

Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni leo ameshutumu  uamuzi wa Benki ya Dunia kusitisha ufadhili mpya ikiwa ni majibu kwa  sheria kali ya kupinga mapenzi ya jinsia moja nchini Uganda.

Museveni ameahidi kutafuta vyanzo mbadala vya fedha.

Uganda itathmini bajeti yake ili kuziba mwanya unaoweza kujitokeza kutokana na hatua hiyo ya Benki ya Dunia.

Benki ya Dunia imesema Jumanne kwamba sheria hiyo ambayo imeweka adhabu ya kifo kwa baadhi ya kwa vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, inapingana na thamini zake na kwamba itasimamisha kwa muda ufadhili mpya mpaka itapoangalia hatua za kuzuia ubaguzi kwa miradi ambayo wanaifadhili.

Benki ya dunia ilikuwa imetenga dola bilioni 5.2 kwa ajili ya uganda licha ya kwamba miradi hii haitaathiriwa.

Sheria la LGBTQ ilipitishwa mwezi Mei imezusha ukosoaji mkubwa kutoka ma taasisi za ndani na kimataifa za haki za binadamu pamoja na serikali za Magharibi ingawa ni maarufu zaidi ndani ya nchi.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii zinatokana na shirika la habari la Reuters