Rais wa Iran Ebrahim Raisi anatakiwa kukamatwa akikanyaga ardhi ya Uswizi

Rais wa Iran, Ebrahim Raisi katika picha iliyochukuliwa October 28, 2023. (Photo by Handout / Iranian Presidency / AFP) / RESTRI

Malalamiko ya kisheria dhidi yake yaliyoonekana na shirika la habari la AFP yalichapishwa Jumatatu. Yaliwasilishwa na watu watatu wanaodaiwa kuwa waathirika wa ukandamizaji wa Iran dhidi ya wapinzani katika miaka ya 1980.

Malalamiko ya kisheria Jumatatu yaliitaka mamlaka ya Uswizi kumkamata rais wa Iran wakati wa ziara iliyotarajiwa na kumfungulia mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu uliohusishwa na kukamatwa kwa wapinzani mwaka 1988.

Malalamiko hayo yanamtaka mwendesha mashtaka wa serikali ya Uswizi, Andreas Muller kuhakikisha kukamatwa na kushtakiwa kwa Rais wa Iran Ebrahim Raisi, kuhusiana na ushiriki wake katika vitendo vya mauaji ya kimbari, mateso, mauaji ya kiholela na uhalifu mwingine dhidi ya ubinadamu.

Raisi alitarajiwa kushiriki katika Kongamano la Kimataifa la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, linaloanza Jumatano mjini Geneva, lakini Umoja wa Mataifa ulisema Jumatatu jioni kwamba Waziri wa Mambo ya Nje, Hossein Amirabdollahian ataongoza ujumbe wa Iran, ishara ambayo Raisi huenda asiwepo.

Malalamiko ya kisheria dhidi yake, yaliyoonekana na shirika la habari la AFP, yalichapishwa Jumatatu. Ofisi ya mwendesha mashtaka haikuthibitisha mara moja kwamba ilipokea. Yaliwasilishwa na watu watatu wanaodaiwa kuwa waathirika wa ukandamizaji wa Iran dhidi ya wapinzani katika miaka ya 1980.