Rais wa Iran afanya ziara kwenye mataifa ya Latin Amerika

Rais wa Iran Ibrahim Raisi (Kushoto), akiwa na mwenzake wa Venezuela, Nicolas Madura mjini Caracas, Jumatatu.

Rais wa Iran Ebrahim Raisi Jumatatu akiwa katika ziara rasmi nchini Venezuela amesema kwamba mataifa yote mawili yana maslahi sawa, pamoja na mahasimu wale wale.

Raisi ambaye alikutana na rais wa Venezuela Nicolas Maduro alisema kwamba mataifa yao yanalenga kuimarisha biashara kutoka takriban dola bilioni 3 kila mwaka hadi dola bilioni 20 kila mwaka.

Mataifa yote mawili yanakabiliwa na vikwazo vikali kutoka Marekani. Viongozi wote wawili wakati wa kikao chao walitia saini mikataba kadhaa ya kibiashara ikiwemo ile ya ushirikiano kwenye uchimbaji madini pamoja na utengenezaji wa kemikali zitokanazo na bidhaa za mafuta.

Rais yupo kwenye ziara ya mataifa shirika ya Latin amerika, wakati ambapo atafanya ziara ya Cuba pamoja na Nicaragua.