Rais Volodomyr Zelenskyy atoa wito kwa Umoja wa Ulaya kuhakikisha kuwa marufuku ya kile alichokiita “isiyokubalika na dhahiri kuwa sio ya Ulaya ya kupiga marufuku nafaka za Ukraine katika nchi tano yanaondolewa na tarehe ya mwisho ya katikati ya Septemba.
Nchi hizo tano za Ulaya ya kati zinataka marufuku ya umoja wa Ulaya kuongezwa walau hadi mwisho wa mwaka. Marufuku hiyo imepangwa kuisha Septemba 15.
Katika hotuba yake ya usiku kwa njia ya video aliyoitoa baada ya mkutano na maafisa wa serikali, Zelenskyy alisema hakuwezi kuwa na suala la kuongeza vizuizi baada ya tarehe ya mwisho.
Tunaamini kuwa upande wa Ulaya utatimiza wajibu wake kuhusu tarehe hii, wakati vikwazo vya muda vitakoma kutumika," Zelenskyy alisema.