Rais William Ruto wa Kenya siku ya Jumapili ameungana na viongozi wengine wa Afrika katika Mkutano wa Tano wa Uratibu wa Katikati ya Mwaka (5th MYCM) wa Umoja wa Afrika, Jumuiya za Kiuchumi za Kikanda, Taratibu za Kikanda. Kulingana na taarifa katika vyanzo mbalimbali ikiwemo gazeti la The Star la Kenya.
Mkutano huo umeitishwa chini ya kauli mbiu ya AU ya mwaka 2023 “Kuharakisha Utekelezaji wa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA)”. Marais 10 wa Afrika waliwasili nchini Kenya Jumamosi usiku, akiwemo mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni Rais wa Comoro, Azzali Assoumani. Wengine ni Ali Bongo wa Gabon, Abdel Fattah wa Misri, Macky Sall wa Senegal, Ismail Omar Guelleh wa Djibouti, na Bola Ahmed Tinubu wa Nigeria.