Rais wa Marekani Barack Obama, anatazamiwa kuomba kuongezeka kwa ushuru kwa Wamarekani matajiri katika hotuba yake ya kila mwaka juu ya hali ya kitaifa.
Rais Obama atalihutubia Bunge la Marekani siku ya Jumaanne usiku kwa saa na Marekani Mashariki.
Bunge la Marekani kwa sasa ni la kwanza lenye wapinzani Waripublican wengi katika kipindi chote cha uongozi wa Rais Obama.
Rais Obama ataomba kuongezeka kwa ushuru wa faida za watu wanapouza mali zao kama vile hisa, biashara ya kuuza nyumba na ardhi.
Pia mapendekezo ya Rais Obama vilevile yatahusu kutoza ushuru wa mauzo ya nyumba ya kurithiwa yenye thamani ya mamilioni ya dola, pamoja na mashirika makubwa ya kifedha nchini Marekani.