Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, dawa ya kulevya aina ya Kush, inayotengenezewa viwandani, na yenye athari sawa na bangi, imeshamiri zaidi miongoni mwa vijana nchini Liberia, pamoja na jirani wake Sierra Leone.
Ni rahisi kutambua watumizi wake kutokana na ulevi wa aina yake, wakati wakionekana kwenye mitaa ya mabanda pamoja na ile ya kifahari. Boakai wakati wa hotuba yake ya dakika 40 mbele ya bunge, alisema kwamba yeye na naibu wake watakuwa wa kwanza kufanyiwa vipimo vya dawa, tangazo lililokaribishwa kwa furaha na wabunge.
“Utumizi wa dawa za kulevya na hasa Kush nchini mwetu, ni tishio kubwa kwa watoto wetu pamoja na taifa kwa ujumla,” aliongeza Boakai. Rais wa zamani George Weah aliyeshindwa na Boakai kwenye uchaguzi wa Novemba, wakati wa kampeni alikosolewa pakubwa kwamba alishindwa kukabiliana na tatizo hilo.