Rais Tayyip Erdogan aliashiria Jumatano kwamba uchaguzi utafanyika Mei 14 akishikilia mpango wake wa awali wa kupiga kura akitaja tarehe, zaidi ya miezi mitatu baada ya tetemeko kubwa la ardhi kuwaua zaidi ya watu 45,000 nchini Uturuki. "Taifa hili litafanya kile kinachohitajika Mei 14, Mungu akipenda," Erdogan alisema katika hotuba yake kwa wabunge kutoka chama chake tawala cha AK bungeni.
Kumekuwa na ishara zinazokinzana kuhusu uwezekano wa muda wa uchaguzi wa urais na ubunge tangu tetemeko la ardhi la mwezi uliopita huku wengine wakieleza kuwa huenda uchaguzi ukaahirishwa hadi baadaye mwaka huu au usifanyike kama ilivyopangwa Juni 18.
Kabla ya mkasa huo umaarufu wa Erdogan ulikuwa umeporomoka kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha na kushuka kwa sarafu ya Uturuki ya Lira. Tangu wakati huo amekuwa akikabiliwa na wimbi la ukosoaji kufuatia hatua ya serikali yake kukabiliana na tetemeko baya la ardhi kuwahi kutokea katika historia ya taifa hilo.